Podchaser Logo
Home
MIMI NIPUNGUE by Mwl Onorodgers

MIMI NIPUNGUE by Mwl Onorodgers

Released Tuesday, 19th September 2023
Good episode? Give it some love!
MIMI NIPUNGUE by Mwl Onorodgers

MIMI NIPUNGUE by Mwl Onorodgers

MIMI NIPUNGUE by Mwl Onorodgers

MIMI NIPUNGUE by Mwl Onorodgers

Tuesday, 19th September 2023
Good episode? Give it some love!
Rate Episode

MIMI NIPUNGUE WEWE UONGEZEKE

Yohana 3:25 Basi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja juu ya utakaso. 26 Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng’ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea. 27 Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni. 28 Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. 29 Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. 30 Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.

=>Haya maneno inawezekana tumewahi kuyasema mara kadhaa kumwambia YESU aongezeke na sisi tupungue....

Au mara nyingine tumetumia maneno haya “YESU jitwalie utukufu na mimi sichukui hata chembe ya utukufu

Mambo gani ya kujifunzaa?1)-YESU anapochukua nafasi ni kweli kila kitu kinabadilika; yaani unapompatia yeye nafasi ni lazima utegemee mabadiliko

2)Lazima uwe tayari kwa hayo mabadiliko yatakayo mpatia yeye kuongezeka na wewe kupungua

=>Tunafikiri kuongezeka ni lazima iwe imetokea ndani yetu na kumbe si hivyo anaweza akaongezeka lakini si kupitia wewe hapo ofisini,hapo kazini,hapo mtaani au kwenye hiyo huduma.Ila wewe hauko tayari

Mfano; unampa YESU KRISTO nafasi hapo kazini kwenu na unaingia kwenye maombi ya mzigo sana juu ya changamoto mnayoipitia hapo ofisini au kwenye huduma au biashara,na saa nyingine anakupa hata maelekezo ya namna ya kuomba na hata SADAKA ya kutoa.......Halafu kweli anaingilia kati yeye YESU na kuondoa ile shida lakini sifa anapewa kiongozi wako na si wewe,Sifa anapewa yule mwenzio ambaye ni mtesi wako hapo ofisini na si wewe,Sifa anapewa yule mpinzani wako kwenye fellowship na si wewe,

Nini nachotaka tujifunze?Ni kweli YESU KRISTO anaweza kuongezeka na wewe ukapungua ila hatukotayari kuona hilo maana ndani yetu bado kuna roho ya mashindano na sio roho ya kuujenga ufalme wa MUNGU tunataka YESU aongezeke na sisi tuongezeke hapo hapoo

KWANINI NI MUHIMU KUELEWA JAMBO HILI?

1)-Kazi ya MUNGU acha ibaki kuwa ya MUNGU ni sio yakwako hata kama MUNGU alikutumia kwa machozi na gharama kubwa hapo kabla wakati haionekani....

Ikishatimia na kuonekana unaweza hata usitambulike au kutambulishwa jinsi ulikuwa na bidii na hiyo kazi KISIKUMBUE mwachie mwenye kazi aongezeke wewe upungue

Saa nyingine utasemwa kwa aibu ili uondolewe hashima yote na kufedheheshwa kabisaa...ZIDI KUPUNGUA ILI YEYE AONGEZEKE

Unaweza kujiuliza swali kwanini YESU KRISTO aruhusu hivyo?

JIBU;Kunawakati YESU KRISTO anatako uondoke kwenye picha,sport light (mstari wa mbele) ili aendelee kukutumia vyemaa.

Unaweza usijue lakini kupungua kwako ndio njia YESU KRISTO ameitumia kukuondoa kwenye kisasi cha adui baada ya hiyo kazi MUNGU alikutumia.....saa nyingine ni yeye amekuficha ACHA WAONEKANE WENGINE wewe baki ukimtukuza YESU KRISTO

Show More

Unlock more with Podchaser Pro

  • Audience Insights
  • Contact Information
  • Demographics
  • Charts
  • Sponsor History
  • and More!
Pro Features