Podchaser Logo
Home
Yohana 1:19-34

Yohana 1:19-34

Released Saturday, 19th October 2019
Good episode? Give it some love!
Yohana 1:19-34

Yohana 1:19-34

Yohana 1:19-34

Yohana 1:19-34

Saturday, 19th October 2019
Good episode? Give it some love!
Rate Episode

Roho Mtakatifu Wa Ajabu

Yohana 1:19-34

Utangulizi

      Somo moja katika biblia ambalo si rahisi sana kwa wakristo ni somo kuhusu Roho Mtakatifu. Ni wakristo wachache sana ambao hawana wasiwasi wowote kuhusu hii nafsi ya Tatu ya Mungu. Inawezekana hali hii inatokana na kukosa uelewa.

Hali hii ya kukosa uelewa inaweza kufananisha na mtoto ambaye hajaonana na mamake kwa miaka 15. Anapokutana na mamake, anachanganyikiwa hajui amkumbatie au ajifiche kutoka kwake. Mtoto anajua inampasa ampende mamake lakini hana uhakika.

Vivyo hivyo, watu wengi hawana uhakika jinsi wanavyoweza kuhusiana na Roho Mtakatifu. Tunajua Roho Mtakatifu alikuja akiwa na furushi nzima la ukombozi wetu lakini tuna wasiwasi kufungua sehemu hii ya furushi hili.  

Kwa sababu hiyo ninapenda kuchukua muda wa kutosha ili nishughulikie somo hili kuhusu ubatizo wa Roho Mtakatifu. Kwa hakika somo hili litatupeleka katika maeneo mengi – litajibu maswali mengi na pia maswali mengi yatajitokeza.

Basi Fungua Biblia yako katika injili ya Yohana, sura ya 1

Ubatizo wa Yohana

Yohana alizungumzia ubatizo wa Roho Mtakatifu, aliowahubiria watu wake. Huyu ni Yohana gani tunayemzungumzia? Kumbuka ya kwamba hapa tunazungumzia kina Yohana wawili tofauti. Yohana aliyeandika Injili ya Yohana, na Yohana Mbatizaji, ambaye habari zake zimeandikwa na Yohana mwandishi wa Injili pamoja na waandishi wa Injili nyingineno, yaani Mathayo, Luka na Marko. Hapa tunazungumzia Yohana mbatizaji.

Hebu tusome mstari wa 19 hadi 25.

Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, wayahudi walipotuma kwake makuhani na walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, wewe u nani? Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, mimi siye Kristo. Wakamwuliza, ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, la. Basi wakamwambia, U nani? tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? Akasema, mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya. Na wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa mafarisayo. Wakamwuliza, wakamwambia, mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?

Kwa uelewa wa wayahudi, “ubatizo” kwa kiyunani “baptize” lilikuwa ni jambo la kawaida kabisa, na maana yake ni kuzamisha. Ubatizo ulifananishwa na kuzamisha kitambaa kwenye rangi. Kwanza kitambaa kiliwekwa kwa jiki kukisafisha na baadaye kilitumbukizwa kwa rangi ili kupata rangi iliyokusudiwa. Kwa myahudi ubatizo ulikuwa na maana ya kutakasika na kutia wakfu  kwa ajili ya utambulisho mapya.

Msikizaji wangu, maji pia yalitumika katika agano la Kale katika sherehe za utakaso. Kulingana na walawi, mtu aliye najisi au mchafu ilimbidi mtu huyo ajioshe kwa maji kabla ya kurejesha ndani ya ushirika wa walioamini.

Vivyo hivyo, Yohana alikuja akitangaza toba na ubatizo – sherehe ya kusafishwa kwa maji. Mtu hangeweza kumfuata Yohana pasipo kwanza kuamini ujumbe wake na kubatizwa – mawili haya yalikuwa muhimu. Ni kama vile mtu hangeweza kuwa muamini katika sheria ya Musa bila kutahiriwa.

Hebu na tusome Marko sura 1, mstari wa 4 na 5

Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalem wote, wakabatizwa katika mto Yordani, wakiziungama dhambi zao.

Na je, Ujumbe wa huyu nabii ulikuwa nini? Tusome mstari wa 8

Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa roho Mtakatifu.

Ni vema tuelewe kwamba ubatizo wa Yohana ni tofauti sana na ubatizo wa walioamini. Ingawa tunasoma vitabu vya injili kama Marko, Yohana, Luka na Mathayo katika Agano Jipya, bado tuko katika Agano La Kale na Yohana ni nabii wa Agano La Kale.

Ama kwa kweli, wale walioufu

Support the show (https://www.patreon.com/tumaini_imara)

Show More
Rate

Join Podchaser to...

  • Rate podcasts and episodes
  • Follow podcasts and creators
  • Create podcast and episode lists
  • & much more

Episode Tags

Do you host or manage this podcast?
Claim and edit this page to your liking.
,

Unlock more with Podchaser Pro

  • Audience Insights
  • Contact Information
  • Demographics
  • Charts
  • Sponsor History
  • and More!
Pro Features